} });
 

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amejiuzulu nafasi ya kiongozi wa Chama cha Conservative. 

Boris amejiuzulu nafasi hiyo jana Alhamisi Julai 7, 2022 lakini bado atabaki kuwa Waziri Mkuu mapaka chama hicho kitakapopata kiongozi mpya mwezi Oktoba. 

Katika hotuba yake, Boris amesema “Nina huzuni kuacha kazi bora zaidi duniani. 

Ninataka ujue jinsi ninavyohuzunishwa na kuacha kazi bora zaidi duniani,’’

"Nimekubaliana na Sir Graham Brady, mwenyekiti wa wabunge wetu wa viti maalum, kwamba mchakato wa kumchagua kiongozi mpya uanze sasa na ratiba itatangazwa wiki ijayo. Na leo nimeteua Baraza la Mawaziri kuhudumu, pia nitaendelea kuongoza hadi kiongozi mpya atakapochaguliwa.’’ 

Amejiuzulu baada ya kuhudumu katika wadhifa huo chini ya miaka mitatu, licha ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa 2019. 

Kinachofuatia baada ya kiongozi huyo wa Conservative kujiuzulu, uchaguzi wa kiongozi mpya wa chama unaanzishwa ambapo chini ya sheria za sasa, wagombea wanahitaji kuungwa mkono na wabunge wanane wa chama hicho ili kuwania.  

Baada ya wagombea wote kuidhinishwa na iwapo ni zaidi ya wagombea wawili, wabunge wa chama hicho watashiriki katika uchaguzi hadi wagombea wawili watakaposalia. 

Katika raundi ya kwanza, mgombea ni sharti ajipatie asilimia 5 ya kura ili kusalia katika kinyanganyiro. 

Katika raundi ya pili ni sharti wajipatie asilimia 10 ya kura. 

Katika raundi itakayofuata mgombea mwenye kura kidogo ataondolewa.

Wakati wabunge wawili watakaposalia, wanachama wote wa chama cha Conservative nchini na sio wabunge watampigia kura mshindi.

Muda wa uchaguzi huo huamuliwa na kamati ya kamati ya wabunge wa nyuma na kamati hiyo itapiga kura kubadilisha sheria kabla ya uchaguzi huo kufanyika.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top