} });
 

 

Rais mpya wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe amewaalika rasmi wabunge kujiunga na serikali ya umoja wa vyama vyote ili kufufua uchumi uliofilisika wa nchi hiyo kwa kufanya mageuzi magumu.

Akizungumza katika mkutano na watawa wenye ushawishi mkubwa wa Hekalu la Jino huko Kandy, moja ya madhabahu matakatifu zaidi ya kibuddha, Wickremesinghe alisema angependa kuanza safari mpya ya kuvileta vyama vyote pamoja na kuendeleza safari hiyo kuunda serikali ya vyama vyote.

Amewaandikia wabunge wote kuwataka kujiunga na serikali hiyo ya umoja. Wickremesinghe alichukuwa uongozi mapema mwezi huu baada ya ghadhabu ya umma kuhusu mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi katika taifa hilo kumlazimu mtangulizi wake Gotabaya Rajapaksa kuikimbia nchi hiyo na kujiuzulu.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top